MALEZI YA MTOTO

Wote tumekuwa tukitaka kuwa wazazi bora kwa watoto wetu lakini ushauri umekuwa mwingi katika kuwakuza watoto ili wawe na uwezo wa kujiaamini, rafiki na mwenye mafanikio. Ni muhimu sana kuweka uwiano katika vipaumbele, majukumu, mahitaji muhimu ya mtoto wako, wanafamilia wengine na wewe mwenyewe. Hapa tutajadiliana jinsi gani tunaweza kuwasaidia watoto wakue na kuwa, wewe kama mzazi unataka bila kupotea wakati wa malezi ya watoto wetu.

Malezi ya watoto ni nini?

Malezi ya watoto ni hatua za kuwakuza watoto na kuwapatia ulinzi wa kutosha unaoambatana na kujali ili kuhakikisha wanapokuwa watu wazima wawe waliokuwa bora.

Malezi mazuri ya watoto ni yapi?

Malezi mazuri ya watoto ni yale yanayohusisha uthabiti, ratiba na kuwapatia watoto hisia ya kudhibiti. Malezi mazuri ya watoto humpa mtoto uhuru katika kukua na kuwalea watoto kwa kuzingatia umri wa mtoto na hatua ya ukuaji aliyofikia.

Malezi mazuri ya watoto

Aina ya malezi ya watoto.

Kitu kimoja kinachotia hamasa kuwa mzazi ni utofauti jinsi tunavyokuza watoto wetu. Na wakati huohuo kuna vitu vingi vimezoeleka kutoka kwa wazazi tofauti. Watafiti wamejaribu kueka makundi manne ya malezi kutokana na jinsi wazazi wanavyolea watoto wao.

1. Malezi ya kimabavu/ubabe

Malezi ya kibabe

Wazazi uwalea watoto wao katika misingi ya nidhamu, watoto hutakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu na akifanya kosa la utovu wa nidhamu ni lazma kuadhibiwa vikali na wazazi. Mzazi ndiye kila kitu katika makuzi ya mtoto, hueka sheria na nakutoa amri kwa mtoto bila kumpa nafasi na ata maelezo kwa watoto. Watoto hulelewa katika mazingira ya ukali sana na kupangiwa kila kitu na wazazi. Hakuna mawasiliano ya kutosha kati ya wazazi na watoto. Matarajio kutoka kwa watoto ni makubwa lakini yasiyo kuwa uhuru. Mfano; Mtoto anaweza akawa na ndoto ya kuwa mchoraji wazazi wakataka ni lazima awe rubani.

2. Malezi ya kudekeza

Malezi ya kudekeza

Wazazi uwalea watoto kwa kuwaacha wafanye wanachokitaka na kuwapatia muongozo kidogo sanawa kile wanachokifanya. Wazai huwa marafiki zaidi kwa watoto kuliko wazazi, husimamia nidhamu wastani na si kwa hali ya juu. Watoto hugundua na kutatua matatizo yao wao wenyewe na pia mtoto huusishwa katika maamuzi na ata kufanya maamuzi yao wenyewe na sio kutoka kwa wazazi. Mawasiliano huwa ni makubwa kati ya mtoto na wazazi na mara nyingi yanaweza yakawa yakupitiliza. Matarajio kutoka watoto ni madogo na mara nyingi anayajua mtoto mwenyewe. Mfano; Watoto wa shule ya sekondari wasiopeleka ripoti zao za matokeo kwa wazazi ni wao wenyewe ndo wanajua wanatarajia kupata matokeo ya aina gani katika mitihani yao ya kumaliza elimu yao ya sekondari.

3. Malezi huru

Malezi huru

Wazazi huwapa watoto uhuru uliopitiliza, watoto hurura mitaani na wazazi hajui ata watoto wako wapi. Wazazi hawajui watoto wao wamekula nini, wamevaa nini na hata wapi wamelala. Wazazi hawana mda na malezi ya watoto na hata kujua wafanye nini katika malezi ya watoto. Hakuna nidhamu katika aina hii ya malezi ya watoto, watoto huachwa wafanye chochote wanachokitaka bila muongozo wowote. Hakua mawasiliano kati ya wazazi na watoto na kama yapo ni madogo sana. Matarajio kutoka kwa watoto ni machache sana au yasiwepo kabisa. Mfano; Watoto wanaweza wakawa hawafiki shuleni lakini wazazi wakawa hawana taarifa kwa sababu hawatengi muda wa kwenda kufuatilia maendeleo ya mtoto shuleni.

4. Malezi ya muafaka

Malezi muafaka

Wazazi huwa na busara, walezi na hupanga matokeo ya hali ya juu na matarajio kutoka kwa watoto. Watoto huwa na nidhamu na kujitunza wenyewe. Sheria za nidhamu huelezewa kwa sababu gani zimewekwa. Aina hii ya malezi ndio inafaa zaidi kwa watoto. Mazungumzo ni mara kwa mara na yanayoendana na umri/uelewa wa watoto. Matarajio kutoka kwa watoto ni makubwa lakini yanayotambulika. Watoto wanaweza kuwa sababu ya matarajio yao.

Je ni aina gani ya malezi ya watoto ninayotumia?

Wachache wetu hutumia aina moja ya malezi ya watoto, lakini ni vizuri kuwalea watoto kwa aina mbalimbali za malezi ya watoto. Mfano; Wazazi anaweza asitumie malezi ya ubavu, lakini nyakati katika malezi ya watoto inahitajika atumie aina hiyo ya malezi ya watoto.

Wakati ni rahisi kumlea mtoto pale wazazi wanapotumia aina moja ya malezi, baadhi ya utafiti unaonyesha kama mzazi mmoja akitumia malezi ya kimabavu itamsaidia mtoto zaidi kuliko wote watumie malezi ya kudekeza.

Kama umefurahishwa na chapisho hili, tafadhali sambaza kwa ndugu, jamaa na marafiki!

2 thoughts on “MALEZI YA MTOTO

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started