
Mzazi mmoja hulea mtoto/watoto bila msaada wa mwenzi, athari ya malezi ya mzazi mmoja kwa mtoto inaweza kuwa nzuri au mbaya. Maisha katika nyumba ya mzazi mmoja, japokuwa yamekuwa ni ya kawaida katika familia zetu za kileo yanaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mzazi na mtoto. Katika familia za kileo malezi ya mzazi mmoja yamekuwa ya kawaida sana katika jamii zetu kuliko familia zenye Baba, Mama na Watoto. Maisha katika nyumba zenye malezi ya mzazi mmoja yanaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mzazi na mtoto. Mzazi anaona amezidiwa na majukumu ya kulea mtoto, kufanya kazi, kulipa bili mbalimbali,ada na kazi za nyumbani. Na wakati mwingine vyanzo vya pesa hupungua pale mzazi anapobaki mwenyewe kulea watoto. Familia zenye malezi ya mzazi mmoja mara nyingi hukutana na matatizo mbalimbali ambayo yanaweza yasiwakute familia nyingine.
Matatizo yanayotokea kwenye familia ya malezi ya mzazi mmoja
Licha ya athari ambazo hutokana na malezi ya mzazi mmoja watoto wanaweza kuwa wenye furaha na mafanikio. Kwa uangalifu zaidi, mzazi mmoja anaweza kulea mtoto mwenye mafanikio na maendeleo bora ya jumla katika maisha yeao ya kijamii na kihemko

- Matokeo ya ugomvi unaoendelea kati ya wazazi wawili
- Wazazi na watoto kukosa mda wa kujumuika kwa pamoja
- Matokeo mabaya shuleni baada ya wazazi kutengana
- Matatizo yanayotokea baada ya wazazi kuanzisha mahusiano mengine
- Maelewano mabaya katika familia
Mzazi anayelea mtoto peke ake anaweza kusaidiwa na wanafamilia kwa kuongelea hisia zao na kushilikiana kwa pamoja kutatua matatizo. Kupata msaada kutoka kwa marafiki, wanafamilia na watu wa dini. Matatizo yakizidi ni salama kuwaona madaktari wa afya ya akili.
Athari nzuri za malezi ya mzazi mmoja
Wakati unasikia juu ya athari mbaya ya malezi ya mzazi mmoja yanaweza kuwa mazito, pia Kuna athari nzuri kwa watoto waliolelewa na mzazi mmoja
- Mahusiano yalibora kati ya mzazi na mtoto
- Kushiriki kwa pamoja katika majukumu ya familia
- Mwingiliano wa uzoefu na jamii halisi
- Ukomavu wa mzazi na mtoto kuhakikisha familia ipo vizuri
Malezi ni kazi ngumu. Wazazi wote kuna wakati wanakasirika na kufadhaika. Lakini usitoe hisia zako juu ya mtoto wako. Ukianza kuhisi kuzidiwa, kuna vitu unaweza kufanya ili usijisikie kuzidwa
- Kubali msaada
- Tafuta mda kwaajili yako na mtoto wako
- Furahiya na mtoto wako
- Tenga wakati kwaajili yako mwenyewe
- Mtafutie mtoto watu wa kuwaiga kama mfano
Hata kama changamoto ni nyingi mzazi mmoja anaweza kulea mtoto mwenye mafanikio. Muoneshe mtoto wako upendo, heshima na muonyeshe mambo chanya ya kuhakikisha kuwa mtoto wako anastawi maishani
