5. MALEZI YA MTOTO WA UMRI WA SHULE

Umri wa shule

Katika kipindi hiki ambacho mtoto ana miaka 3 mpaka 6-7, ukuaji wa mtoto katika kipindi hiki huwa ni mdogo kwasababu nguvu nyingi hutumika katika kupata maarifa kuliko kuongezeka kwa mwili

Ukuaji wa mwili

Urefu huongezeka takribani 5cm kwa mwaka. Mtoto (kike/kiume) huwa na miguu mirefu.

Harakati na vitendo vya misuli

Mtoto wa umri wa shule huanza kuona maendeleo yao katika harakati na vitendo vya misuli. Watakuwa vizuri zaidi katika kudhibiti, kuratibu na usawa. Misuli yao huanza kubadilika katika watoto wa umri wa shule ambayo huwafanya wawe na nguvu za kutosha

Hatua kuu za ujuzi wa kazi

  • Uwezo mkubwa wa harakati na vitendo vya misuli
  • Hisia za ukuaji wa mwili hukua
  • Kujua mwili wake unakimbilia balehe
  • Utofauti wa jinsia hujionyesha

Ukuaji wa akili

Mtoto wa umri wa shule huwa na uwezo wa kuelewa mantiki na habari halisi hasa katika maisha yake binafsi. Mtoto anaweza bado akapambana kufahamu dhana ya kudhani/kufikirika hasa kwa zile zitakazotokea katika kipindi kirefu kijacho. Mtoto wa umri wa shule huanza kufikiria watu wengine na kuwa na uwezo wa kufikiria na kuelewa vitu kutoka katika maoni mbalimbali

Kazi za utambuzi

Mtoto wa umri wa shule anakuwa na uwezo wa kuzingatia kazi/mada. Mtoto ataanza pia kudharau usumbufu wowote wanapokuwa na kazi/mada ya kuzingatia. Uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa mda mrefu au mfupi huanza kuimarika katika kipindi hiki cha umri wa shule. Mtoto wa umri wa shule atakuwa na uwezo wa kuvuta kumbukumbu ya vitu muhimu ( vilivyotokea miezi au miaka iliyopita). Mtoto huwa na uangalizi mzuri, anakuwa na uwezo wa kuzingatia kazi kazi muhimu kwa muda mrefu. Mtoto huanza kusoma vitabu vyenye kurasa nyingi, kuwa na vitu anania navyo shuleni na kujihusisha katika miradi ya muda mrefu

Kuchochea kwa Utambuzi

Kuchochea kwa utambuzi katika kipindi cha umri wa shule, mzazi ampe mtoto vitu chochezi katika utambuzi na michezo yenye changamoto. Mtoto apewe vitabu vingi mbalimbali vyenye makuzi sahihi na tamaduni mbalimbali. Mzazi awe mfano wa kuonyesha umuhimu wa kujali, heshima, ukweli na majukumu. Mtoto apewe nafasi ambayo mtoto wa umri wa shule atapumzika na apewe uhuru mda huo atafanya nini. Mzazi atekeleze shughuli ambazo zitafanywa kwa pamoja zinazoweza kutumia nguvu na uwezo

Hatua za kihemko katika jamii

Umri wa shule mtoto huingiliana na jamii tofauti na nyumbani ambapo hupelekea maadili yanayopingana, japokuwa mtoto huwa makini na yeye mwenyewe hujifunza kwa bidii na kugundua ni kwa jinsi gani watu wanaozunguka huwasaidia katika kukua na kujifunza ( mtoto hujiringanisha na kuchagua marafiki). Maoni hasi ya marafiki huweza huleta kizuizi kikubwa

Mahitaji ya kihemko ya kijamii

Mtoto katika kipindi cha umri wa shule,huanza kujiuliza maswali kama yeye ni nani? Nani anampenda? Mtoto huanza kutambua historia ya familia yake na kuendelea kuelewa yeye ni nani. Mtoto hufanyia kazi suala la maadili na imani lakini pia kuchukua misimamo. Mtoto huanza kujitegemea yeye mwenyewe , mtoto wa umri wa shule hutafuta hongera kutoka kwa watu wazima pale wanapofanya vizuri. Mtoto huwa na wivtu kwa ndugu yake au rafiki ake anayefanya vizuri kumzidi yeye au anayeonekana zaidi kwa wazazi au mtu mzima yoyote

Malezi mazuri ya mtoto

Mzazi mzuri humsaidia mtoto kujiona Hana shida na anapata msaada, kugundua mambo mazuri ambayo mtoto ameyatimiza. Mzazi humueshimu mtoto na kumsikiliza anachokisema na kuyatendea kazi vitu mtoto anavyovipenda, kumkubali na kumpatia hongera. Mzazi mzuri huwa mkweli na hufuatilia anachokisema atakifanyia kazi, lakini pia mzazi humsaidia mtoto kutengeneza mahusiano mazuri na rafiki zake. Mzazi pia anapaswa kumfundisha mtoto kuziendesha hisia zake, kumsaidia kuepuka msongo wa mawazo wakati anatengeneza urafiki

Je! wajua kuwa katika malezi ya mtoto wako lazma uwe na malengo?

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started