
Ujana ni kipindi cha kati ya utoto na ukubwa, huanzia miaka 12 mpaka 18. Vijana hupata mabadiliko ya mwili ambayo huashiria kuwa mkubwa
Ukuaji wa mwili
Mabadiliko haya yanaweza kuwa ya kuchanganya na saa nyingine kutisha. Ni muhimu sana kwa mzazi kufahamu ni mabadiliko gani mtoto huyapata anavyokuwa katika ujana
Mabadiliko kwa wavulana
- Mabadiliko ya homoni ambayo hupelekea mabadiliko ya mwili katika sehemu za siri za kiume
- Kuota nywele kwenye makwapa, sehemu za siri, kifuani na usoni
- Mabega kuwa mapana
- Sauti huanza kubadilika na kuwa nzito
Mabadiliko kwa msichana
- Mabadiliko ya homoni huandaa mwili wa msichana kuanza kupata hedhi
- Kuota nywele chini ya makwapa na sehemu nyingine za siri
- Mwili kaanza kubadilika na kuwa mkubwa wenye shepu kubwa na matiti kuota
Matokeo ya mabadiliko
- Mabadiliko hupelekea ngozi kuwa na mafuta mengi ambayo hupelekea chunusi kwenye ngozi ya kijana
- Mabadiliko hupelekea matatizo ya kutokujiamini kwa kijana
Jamii na muonekano wa mwili wa kijana
- Upatikanaji wa habari kwa urahisi unaweza kumuathiri kijana kuhusu muonekano wake ( mabadiliko) kwenye mwili wake. Mfano; kutaka kuwa kama muigizaji fulani
- Kujiringanisha katika jamii na kutaka kuwa kama mtu fulani kwenye jamii inayomzunguka
- Kuonewa na kutaniwa humshusha mtoto uwezo wake wa kujiamini
Usaidizi wa mzazi
Mzazi anatakiwa azungumze na mtoto na ajaribu sana mazungumzo yawe chana. Mpatie mtoto pongezi na majadiliane kwa pamoja mafanikio, wakati wa maongezi mzazi atambue mawazo hasi na amsaidie mtoto ayaone ni chanya. Mzazi msifie mtoto kwa usahihi ampongeze na kumhimiza. Mzazi msaidie mtoto kuelewa mabadiliko ya mwili wake ambayo hawezi kuyabadilisha yeye. Mzazi hata siku moja asimfananishe mtoto na uwezo wake na marafiki zake, hii inaweza kuwa hatari kwa mtoto akihisi hana uwezo kama marafiki zake
Uwezo wa utambuzi
Kijana anakuwa na uwezo wa kuwaza na kujiandoa. Anauwezo wa kufikiria kwa dhana, kuzingatia uwezekano na kimantiki. Kijana huchukua mitazamo na kuelewa lakini pia kuzingatia mitazamo mingine. Kijana hujiekea zaidi malengo, ukuaji wa akili ya kijana mara nyingi huathiriwa na hali yake ya hisia. Kijana huanza kuelewa sura za ulimwengu wa watu wazima
Mahitaji ya kihemko ya kijamii
Kijana huitaji kutengeneza uhuru wake yeye mwenyewe, lakini pia kujumuika na jamii kwa kiwango kikubwa huka ikiwa ni matarajio makubwa na mahitaji. Kijana kutafuta kukubalika katika kundi la marafiki zake, hufanya maamuzi yake peke ake na yuko tayari kusema hapana. Kijana hujaribu kutengeneza umaarufu wao na sio kutegemea wazazi (Hii inaweza kupelekea ugomvi na wazazi). Kijana huanza kuwa karibu zaidi na marafiki kuliko wazazi kwa ajiili ya msaada, kuanza kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi. Kijana anaweza kumudu hisia zake na kuanza kujikubali
Matatizo yanayoweza kujitokeza
- Kijana kupata msongo wa mawazo uliopitiliza
- Kijana anaweza kujitenga na makundi ya marafiki asiyoendana nayo na kujiweka pamoja na makundi anayofanana nayo
- Kijana kutoweza kujihusisha na masomo
Malezi mazuri
Kijana asaidiwe kuweka malengo yake ya baadae, lakini pia afundishwe jinsi ya kushughulikia mahusiano na kijana wa jinsia nyingine. Kijana apewe nafasi ya kushughulikia maisha yake ya siri. Apewe kazi mbalimbali ili azitumie nguvu zake kwenye kazi za maana
Malezi mabaya
- Tusiwalee vijana kama watoto wadogo
- Tusiwape uhuru uliopitiliza vijana
- Kutomsaidia kijana kujua malengo yake ya baadae
Katika malezi ya mtoto malengo ya mzazi kwa mtoto wake ni muhimu sana, huamua utu uzima wa mtoto
Parenting Tanzania